- 1 -
Al'Imam Nasser Muhammad Al'Yamani
الإمام ناصر محمد اليماني
14 - 08 - 1433 هـ
04 - 07 - 2012 مـ
06:26 صباحاً
https://nasser-alyamani.org/showthread.php?p=50121
ـــــــــــــــــــــ


Mtume wa Mwenyezi Mungu, Lut, swalah na salamu zimshukie, anawakomboa wageni wake kwa binti zake.
نبي الله لوط عليه الصلاة والسلام يفتدي ضيفه ببناته..




ســـــــأل سائل : ما تفسير وبيان هذه الآيات من سورة هود ؟
Muulizaji akauliza: Nini tafsiri na ubainifu wa aya hizi kutoka katika Surat Hud?


Aaudhu Billah Minal Shetani Arajim
{ وَلَمَّا جَاءَتْ رُسُلُنَا لُوطًا سِيءَ بِهِمْ وَضَاقَ بِهِمْ ذَرْعًا وَقَالَ هَـٰذَا يَوْمٌ عَصِيبٌ ﴿77﴾ وَجَاءَهُ قَوْمُهُ يُهْرَعُونَ إِلَيْهِ وَمِن قَبْلُ كَانُوا يَعْمَلُونَ السَّيِّئَاتِ ۚ قَالَ يَا قَوْمِ هَـٰؤُلَاءِ بَنَاتِي هُنَّ أَطْهَرُ لَكُمْ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَلَا تُخْزُونِ فِي ضَيْفِي ۖ أَلَيْسَ مِنكُمْ رَجُلٌ رَّشِيدٌ ﴿78﴾ قَالُوا لَقَدْ عَلِمْتَ مَا لَنَا فِي بَنَاتِكَ مِنْ حَقٍّ وَإِنَّكَ لَتَعْلَمُ مَا نُرِيدُ ﴿79﴾ } صدق الله العظيم
***
Nukuu imeisha


Imam Mahdi Rehema na Amani zimshukie akajibu:
Bismillah Arahman Arahim, Na swala na salamu zimshukie babu yangu Muhammad Mtume wa Mwenyezi Mungu na Aali zake safi na Waislamu wote mpaka Siku ya Qiyaamah. Ama Baada Ya Hayo.


Watu wa Lut walifanya uchafu ambao hawakuwatangulia katika walimwengu kabla yao, na wakapendelea matamanio ya wanaume baina yao pasi na wanawake. Na wakaja wageni wa Ibrahim, rehema na amani ziwe juu yake, badae wakawa wageni wa Nabii wa Mwenyezi Mungu, Lut', akawapokea na akawaingiza nyumbani kwake, akawadhania kuwa ni watu na akauona uzuri wa mandhari. yao. Kwa hiyo aliwaona kama wageni wasiojulikana na kwamba walikuwa Wametoka miji ya mbali, lakini uzuri unaonekana na unapendeza kwenye mndhari yao! Kwa hiyo, Nabii wa Mwenyezi Mungu, Lut, Alingiwa na dhiki nao kwa sababu ya uzuri wao, na aliogopa kwamba watu wake wangewagusa kwa nguvu kwa uchafu. Akasema Allah Ta3ala:
{وَلَمَّا جَاءَتْ رُ‌سُلُنَا لُوطًا سِيءَ بِهِمْ وَضَاقَ بِهِمْ ذَرْ‌عًا وَقَالَ هَـٰذَا يَوْمٌ عَصِيبٌ ﴿٧٧﴾ وَجَاءَهُ قَوْمُهُ يُهْرَ‌عُونَ إِلَيْهِ وَمِن قَبْلُ كَانُوا يَعْمَلُونَ السَّيِّئَاتِ قَالَ يَا قَوْمِ هَـٰؤُلَاءِ بَنَاتِي هُنَّ أَطْهَرُ‌ لَكُمْ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَلَا تُخْزُونِ فِي ضَيْفِي أَلَيْسَ مِنكُمْ رَ‌جُلٌ رَّ‌شِيدٌ ﴿٧٨﴾ قَالُوا لَقَدْ عَلِمْتَ مَا لَنَا فِي بَنَاتِكَ مِنْ حَقٍّ وَإِنَّكَ لَتَعْلَمُ مَا نُرِ‌يدُ ﴿٧٩﴾}
Sadaqa Allah Al’3adhim: [Sura:Hud 77-79].


Na Huenda wale wanaosema juu ya Mwenyezi Mungu wasiyoyajua wakasema: "Nabii wa Mwenyezi Mungu, Lut, rehema na amani ziwe juu yake, aliwatolea watu wake kuwaoa binti zake." Lakini tunatoa fatwa kwa haki na tunasema: Je! wanatosha mabinti zake kwa watu wake kuolewa nao? Basi wao ni wachache na watu wake ni wengi? Muna nini, unahukumu vipi? Kwa hakika, Nabii wa Mungu, Lut alitaka kuwakomboa wageni wake kwa binti zake ili watu wake wapate kumhurumia, kwani jambo lilimjia kuwaletea binti zake ili kutimiza matamanio yao na kutomfedhehesha katika wageni wake.basi ma binti zake ni sahali kuliko wanavyotaka. Lakini watu wa Lut, rehema na amani ziwe juu yake, hawakumwonea huruma licha ya kuwatolea mabinti zake kutimiza matamanio yao na waondoke na wasimfedheheshe katika wageni wake. Lakini hayo mapendekezo hawataki, bali wanataka wanaume ambao ni wageni weny uzuri ambao ni wageni wapya,
Na baada ya kaumu yake kukataa kutimiza matamanio kwa binti zake, wakataka kuwaingia wageni wake, kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu Lut (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akajaribu kuwazuia wasiingie kwa wageni wake, lakini Wakaingia kwa wageni wake kwa nguvu, kisha Nabii wa Mwenyezi Mungu Lut akawaambia watu wake:
{قَالَ لَوْ أَنّ لِي بِكُمْ قُوّةً أَوْ آوِيَ إِلَىَ رُكْنٍ شَدِيدٍ}
Sadaqa Allah Al’3adhim:
[Hud:80].


Lakini Mwenyezi Mungu aliyatia giza macho ya watu wake, na hawakuwaona wageni wake na uzuri wao walipoingia, lakini Lut alikuwa akiwatazama, hivyo alishangaa jinsi watu wake walivyokuwa hawawaoni.


Na alistaajabu kwamba watu wake hawakuwaona wageni wake ingawa walikuwa mbele yao mahali pa kuwapokea wageni, lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyatia kiza macho yao kutokana na kuwaona wageni wa Nabii wa Mwenyezi Mungu Lut. Akasema Allah Ta3ala:
{وَلَقَدْ رَاوَدُوهُ عَن ضَيْفِهِ فَطَمَسْنَا أَعْيُنَهُمْ}
Sadaqa Allah Al’3adhim: [Sura:Al-Qamar].


Lakini Nabii wa Mungu Lut alistaajabishwa na jinsi watu wake hawakuwaona wageni wake, mpaka watu wake walipokwenda na kukata tamaa mbele ya wageni, ndipo alipowaambia wageni wake Nabii wa Mungu Lut:
{قَالَ إِنَّكُمْ قَوْمٌ مُّنكَرُ‌ونَ ﴿٦٢﴾ قَالُوا بَلْ جِئْنَاكَ بِمَا كَانُوا فِيهِ يَمْتَرُ‌ونَ ﴿٦٣﴾ وَأَتَيْنَاكَ بِالْحَقِّ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ ﴿٦٤﴾ فَأَسْرِ‌ بِأَهْلِكَ بِقِطْعٍ مِّنَ اللَّيْلِ وَاتَّبِعْ أَدْبَارَ‌هُمْ وَلَا يَلْتَفِتْ مِنكُمْ أَحَدٌ وَامْضُوا حَيْثُ تُؤْمَرُ‌ونَ ﴿٦٥﴾ وَقَضَيْنَا إِلَيْهِ ذَٰلِكَ الْأَمْرَ‌ أَنَّ دَابِرَ‌ هَـٰؤُلَاءِ مَقْطُوعٌ مُّصْبِحِينَ ﴿٦٦﴾}
Sadaqa Allah Al’3adhim: [Sura:Al-Hijri 62-66].


Ijapokuwa sayari ya adhabu ilikuwa karibu na ardhi katika usiku huo, lakini hawakuiona sayari ya adhabu kwa sababu inaijia ardhi kutoka ncha za mwisho, kwani tutaeleza kwa kina maelezo kuhusu ukweli wa sayari ya adhabu. Katika Kitabu na kuifafanua kwa watu wanaoamini.


Na Salam Ju Ya Mitume Na Alhamdulillah Rabil3alamin..
Ndugu Yenu; Al’Imam Al’Mahdi Nasser Muhammad Al’Yamani..
أخوكم؛ الإمام المهديّ ناصر محمد اليماني.
ـــــــــــــــــــــــــ